Clear answers for your next step.
Explore practical answers to common questions about investing, licensing, compliance, and Tanzania's capital markets.
01 Kupata gawio langu?
Gawio ni faida ambayo analipwa mwanahisa iwapo kampuni imepata faida na kuamua kulipa sehemu ya faida kama gawio. Njia itumikayo kulipa inategemea na kampuni. Kampuni nyingi zinatumia Shirika la Posta pamoja na mabenki. Ni juu ya mwekezaji kuwasiliana na kampuni aliyowekeza na kutoa taarifa muhimu kama vile anwani ya posta pamoja na akaunti ya benki. Kama malipo yatalipwa kwa kupitia njia ya posta basi utapata Hawala ya Posta kupitia anwani yako, na kama malipo yanafanyika kupitia kwenye akaunti ya benki basi utapata hundi au pesa zitaingizwa kwenye akaunti yako. Ni muhimu kutoa taarifa iwapo anwani au akaunti yako itabadilika. Kampuni nyingi zilizoorodheshwa kwenye soko la hisa zinatoa gawio mara mbili kwa mwaka.
02 Kuwa mwekezaji makini?
Sisi kwenye Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana tunaamini kwamba uelewa wa mwekezaji unapaswa kutangulia uamuzi wa kuwekeza na kwamba ufahamu ni njia nzuri sana ya kumlinda mwekezaji. MWEKEZAJI MAKINI husoma taarifa muhimu za vitega uchumi alivyonavyo au anavyokusudia kuwekeza. Vilevile hutafuta ushauri wa uwekezaji toka kwa Washauri wa Uwekezaji, Wachuuzi, Madalali wa DSE na wataalamu wengine wenye leseni zinazohusika.
MWEKEZAJI MAKINI katika masoko ya mitaji anajua haki zake na anaelewa jinsi masoko ya mitaji yanavyofanya kazi. Ni muhimu kwa mwekezaji kujua mambo ya msingi na taratibu za bidhaa anazonunua kupitia masoko ya mitaji. MWEKEZAJI MAKINI hujifunza kuhusu masoko ya mitaji.
Mpango wa Kuwekeza
Kushinda vita ni lazima uwe na mpango wa vita. Ili kufanya ndoto zako za uwekezaji kuwa kweli, unahitaji mpango wa uwekezaji. Mipango ya uwekezaji humsaidia MWEKEZAJI MAKINI kupanga malengo yake ya kifedha na kufanyia kazi mpango huo ili kufikia malengo yake. Kuwa MWEKEZAJI MAKINI kwa kupanga shughuli zako za uwekezaji.
Hatari, Faida na Mwekezaji
MWEKEZAJI MAKINI huwa mwangalifu na hufikiria kuhusu hatari ya kupata hasara katika hatua yoyote ya faida. Kwa ujumla jinsi uwezekano wa kupata faida kubwa unavyoongezeka ndivyo jinsi hatari ya kupata hasara inavyokuwa kubwa pia. Kabla ya kutafuta vitega uchumi ambavyo vinaelekea kutoa faida kubwa fikiria hatari ya kupata hasara unayoweza kukumbana nayo pia.
MWEKEZAJI MAKINI haweki mayai yake yote kwenye kikapu kimoja. Njia mojawapo ya kupunguza hatari ya kupata hasara katika uwekezaji ni kuwa na mseto wa vitega uchumi kwa kuwekeza kwenye rasilimali tofauti.
Simamia Vitega Uchumii Vyako
Mpango wa uwekezaji unapopangwa na kutekelezwa haupaswi kuachwa bila kusimamiwa. Unatakiwa kuwa macho na mseto wako wa uwekezaji ili kujua maendeleo yake na ikiwa unahitaji marekebisho kulingana na hali halisi ya soko au maisha yako yanavyobadilika. MWEKEZAJI MAKINI siku zote anapanga lini aingie, atoke au abakie kwenye uwekezaji.
03 Kuorodhesha hisa za kampuni yangu DSE?
Mchakato wa kuorodhesha hisa huhitaji mwongozo wa kitaalam. Kanuni za Mamlaka (CMSA) na Soko la Hisa la Dar-es-Salaam (DSE) zinaelekeza kuwa kila anayetaka kutoa hisa au hatifungani kwa umma inabidi ateue dalali mdhamini au mshauri mteule kwa ajili ya kudhamini toleo hilo jipya au kuorodheshwa. Dalali mdhamini au mshauri mteule ataisaidia kampuni katika kutimiza masharti yanayotakiwa kwa kuzingatia mambo mbalimbali kama vile iwapo hisa za kampuni husika tayari ziko kwenye mikono ya umma au ni hisa mpya. Dalali mdhamini ataiongoza kampuni inayotaka kuuza hisa kwa umma na kuorodheshwa kwenye safu kuu ya soko la hisa (MIMS); na mshauri mteule ataiongoza kampuni inayotaka kuuza hisa kwa umma na kuorodheshwa kwenye safu ya soko la kukuza kampuni na ujasiriamali ya soko la hisa(EGM). Aidha kampuni zinazotaka kuuza hisa kwa umma na hatimaye kuorodheshwa katika safu hizi mbili, zinatakiwa kuwa na sifa fulani na kutimiza masharti yaliyoainishwa na Sheria ya Masoko ya Mitaji na dhamana na taratibu za Soko la Hisa la Dar es Salaam.
Kukusanya Mtaji kwa Umma na Kuorodheshwa kwenye Safu Kuu ya Soko la Hisa (Main Investment Market Segment (MIMS))
Masharti
- Kampuni iwe imeandikishwa Tanzania chini ya sheria ya kampuni kama kampuni ya Umma na kuwa na wanahisa wasiopungua 7;
- Kampuni iwe na uzoefu usiopungua miaka mitatu na kuwa na mahesabu yaliyokaguliwa ya miaka mitatu;
- Kampuni iwe na mtaji wa kufanyia kazi (working capital) wa kutosha;
- Kampuni iwe na historia ya kupata faida ya miaka miwili kati ya miaka mitatu wakati wa kuleta maombi ya kuorodheshwa;
- Hisa zake ziwe zinahamishika bila kikwazo;
- Ikubaliane na masharti ya kudumu ya kuwepo kwenye soko la hisa;
- Angalau 25% ya hisa zake ziwe mikononi mwa umma;
- Kampuni iwe na mtaji angalau TZS milioni 200;
- Kampuni iwe na angalau wanahisa 1000; na
- Inatakiwa kuonyesha kuwepo na bodi na uongozi thabiti.
Zingatia: Iwapo kampuni inayoomba kuorodheshwa kwenye soko la hisa ni ya kigeni inatakiwa iwe imeandikishwa Tanzania kama kampuni ya kigeni.
Utaratibu wa Kujiorodhesha
- Kupata ridhaa ya kuuza hisa kwa umma kutoka kwa wanahisa;
- Kuteua timu ya wataalamu watakaoitayarisha kuingia kwenye soko la hisa;
- Kutayarisha waraka wa matarajio kama inavyotakiwa na kanuni za utayarishaji wa waraka wa matarajio;
- Kuteua dalali mdhamini;
- Kuwasilisha kwa Mamlaka (CMSA) na Soko la Hisa (DSE), maombi ya kuorodhesha hisa na dhamana kwa kupitia kwa dalali mdhamini;
- Kupata kibali kutoka kwa Mamlaka na Soko la Hisa ili kuanza kuuza hisa katika soko la awali.
Kukusanya Mtaji kwa Umma na Kuorodheshwa kwenye Soko la Kukuza Ujasiriamali (Enterprise Growth Market, (EGM))
Masharti
Yafuatayo ni masharti kwa kampuni inayoomba kukusanya mtaji kwa umma kwa kuuza hisa na kuorodheshwa katika safu ya EGM:
1.Lazima iwe imesajiliwa kama kampuni ya Umma(Public Limited Company) chini ya Sheria ya kampuni;
2.Hakuna kiwango maalum cha mtaji kinachotakiwa;
3.Historia ya utendaji kazi haihitajiki;
4.Historia ya upatikanaji faida haihitajiki;
5.Kama kampuni haitakuwa na historia ya utendaji kazi, waanzilishihawataruhusiwa kuuza hisa zao katika muda wa miaka mitatu ya mwanzo baada ya kampuni kuwa imeorodheshwa;
6.Kampuni lazima iwe na Mshauri Mteule;
7.Lazima iwe na mpango wa biashara wa miaka mitano na taarifa ya ufundi ya kujitegemea iliyotayarishwa na Mshauri Mteule kuhusiana na matarajio ya upatikanaji faida;
8.Kiwango cha chini cha wanahisa ni 300;
9.Umiliki wa umma kwenye kampuni iliyo kwenye soko hili unatakiwa usipungue 20% ya hisa zilizotolewa;
10.Lazima kutengeneza Waraka wa Matarajio na upitishwe na Mamlaka;
11.Waraka wa Matarajio kwa Ufupi uwekwe kwenye magazeti;
12.Lazima kuwe na Kamati ya Ukaguzi kama mwongozo wa utawala bora wa kampuni unavyotaka;
13.Katiba na Waraka wa kuanzishwa kwa kampuni inabidi itamke ulazima wa kufuata misingi ya utawala bora wa kampuni.
Utaratibu:
Kampuni ambayo imetimiza masharti ya mwanzo ya kuorodheshwa inabidi ifuate utaratibu ufuatao:
1.Kuteua timu ya wataalam washauri (consultants) kuiandaa kampuni kwa ajilikuuza hisa kwa umma na kuorodhesha hisa hizo kwenye soko la hisa;
2.Kuteua Mshauri Mteulekuisimamia kampuni tangu wazo la kutafuta mtaji linapokuja hadi kuirodhesha kwenye soko la kukuza ujasiriamali;
3.Kutengeneza Waraka wa Matarajio kwa ajili ya kuuza hisa kwa umma kama inavyotakiwa na kanuni za Mamlaka na Sheria ya Masoko ya Mitaji na Dhamana;
4.Kampuni inabidi ibakie na Mshauri Mteule kwa kipindi chote ambacho kampuni itakuwa imesajiliwa kwenye soko;
5.Inabidi kuwasilisha kwa Mamlaka (CMSA) nasoko lahisa (DSE) maombi ya kuuza hisa na kuorodheshwa kwenye soko la hisa; na
6.Kupitishwa kwa Waraka wa Matarajio kunaiwezesha kampuni kuanza kuuza hisa zake kwa umma kama ilivyoelezwa hapo juu kwenye soko la awali.
Gharama za Kushiriki kwenye Soko la Kukuza Ujasiriamali
Gharama za ushiriki katika EGM zinahusisha ada za kulipa wataalamu mbali mbali watakoongoza kampuni katika mchakato huo. Wataalamu hao ni pamoja na Mshauri Mteule, Mhasibu, Mwanasheria, Mshauri Mkuu na Wakala wa Matangazo na Uchapishaji wa Matangazo na Toleo. Ada zao hamna viwango maalumu ila ni makubaliano kati yao na kampuni husika. Ada za kuchambua waraka wa toleo za CMSA na ada ya kuorodheshwa DSE zimeainishwa kwenye jedwali hapo chini. Ada hizi zimewekwa nafuu kabisa ili kupunguza mzigo kwa kampuni zinazotarajia kutumia EGM kupata mtaji na kuorodheshwa.
Ada ya Kupitia Waraka wa Matarajio (CMSA)
|
Thamani ya Mtaji |
Ada |
|
TZSbilioni 1 au chini yake |
TZS 1,000,000 |
|
Kati ya TZSbilioni 1 na bilioni 5 |
TZS milioni1 ongeza0.1%ya kiasi kinachozidi TZS bilioni 1 |
|
Kati ya TZS bilioni 5 na 10 |
TZSmilioni5 ongeza0.05%ya kiasi kinachozidi bilioni 5 |
|
Zaidi ya TZS bilioni 10 |
TZS milioni7.5 ongeza0.025%ya kiasi kinachozidiTZS bilioni 10 |
Ada ya kuorodheshwa DSE
|
Ada ya mwanzo ya kujisajili |
0.1% ya thamani ya hisa zinazo orodheshwa (kiasi cha chini TZSmilioni 1 na kiasi cha juu TZS milioni 10) |
|
Ada ya kusajili hisa nyingine |
0.1% ya thamani ya hisa zinazoongezwa (kiasi cha chini TZS milioni 1 na kiasi cha juu TZS milioni 10) |
|
Ada kwa kila mwaka |
0.025% ya thamani ya hisa(kiasi cha chini TZSmilioni 1 na kiasi cha juu TZS milioni 10) |
Kupitishwa kwa waraka wa matarajio kutairuhusu kampuni kuanza kuuza hisa kwa umma kwenye soko la awali.
Kwa taarifa zaidi pakua
04 Kutoa Hatifungani
Soko la hatifungani ni soko la madeni na linahusika na hatifungani zitolewazo na serikali kuu, kampuni na manispaa. Soko hili husaidia Serikali kuu, Serikali za mitaa na kampuni kukusanya mitaji ya muda mrefu ili kujenga miundombinu ya uwekezaji kulingana na matarajio ya muda mrefu. Hatifungani zikishatolewa zinaweza kuorodheshwa kwenye Masoko ya Mitaji. Kuorodheshwa kwa hatifungani huwawezesha wawekezaji kuuza wanapohitaji fedha zao, pamoja na kujua thamani ya hatifungani zao.
Masharti ya Utoaji wa Hatifungani
Kampuni inayotaka kutoa hatifungani inahitaji kukidhi masharti yafuatayo:
- Inatakiwa iwe imeshaorodheshwa kwenye soko la hisa;
- Inabidi itoe hatifungani angalau zenye thamani ya TZS 50 milioni kwenye kundi la hatifungani husika. Mauzo zaidi ya hatifungani kwenye kundi sio lazima yafuate masharti hayo;
- Ni lazima iwe na historia ya kupata faida miaka miwili kati ya mitatu ya karibuni;
- Inatakiwa kufikia uwiano unaokubalika wa madeni na isizidi 400% ya rasilimali ya kampuni. Wastani wa fedha zitokanazo na uendeshaji na thamani ya deni zima iwe angalau 40%;
- Itawasilisha waraka wa matarajio ukiambatana na ripoti ya wahasibu yenye taarifa za miaka mitatu iliyotangulia na ripoti ya Wakaguzi wa mahesabu ya mwaka ulioisha;
- Iwasilishe mtiririko wa fedha angalau kwa miezi 12.
- Iwapo mtoaji hatakidhi masharti haya, atatakiwa kumtafuta mdhamini anayetimizamasharti muhimu ya utoaji wa hatifungani kuidhamini kampuni kuwa iwapo itashindwa kutekeleza masharti, mdhamini atalipia hatifungani hiyo.
- Atatakiwa kuingia mkataba na soko la hisa kwa masharti kama yatakavyobainishwa na soko kwa nia ya kumlinda mwekezaji.
Utaratibu wa Kutoa Hatifungani
Mtoaji wa hatifungani ambaye atakuwa amefikia vigezo vya kuorodhesha hatifungani zake soko la hisa (DSE) ni lazima afuate utaratibu ufuatao:
- Utayarishaji wa waraka wa matarajio kwa ajili ya kuuza dhatifungani kama inavyotakiwa na Kanuni za utoaji wa hisa na dhamana kwa umma;
- Mtoaji wa hatifungani anatakiwa kumteua dalali kiongozi atakayepeleka maombi ya kuingia kwenye soko la hisa kwa Baraza la Soko na kuarifu soko kuwa amemteua dalali huyo;
- Mtoaji wa hatifungani na hisa atapeleka maombi yake Mamlaka (CMSA) na soko la hisa kupitia kwa dalali ili yaidhinishwe na Mamlaka na soko; na
- Waraka wa matarajio uidhinishwe kwa ajili ya kuanza kuuza hatifungani kwenye soko la awali.
Kampuni inayotaka kuingia kwenye soko la hisa inatakiwa kumteua mshauri mkuu ambaye atashirikiana na wataalamu wengine kuandaa Waraka wa matarajio, kutathminisha kampuni na kuwasilisha nyaraka zote kwa Mamlaka ili kupata kibali cha kuuza hisa na hatifungani.